6 Desemba 2025 - 10:46
Lebanon inapaswa kukabiliana kikamilifu na uvamizi wa kibeberu wa utawala wa Kizayuni | Mashahidi walijitolea kwa roho, mali na kila walichokuwa nacho

Lebanon inakabiliwa na uvamizi hatari wa Kizayuni: Akirejea mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel kusini mwa Lebanon, alisema: “Lebanon inakabiliwa na uvamizi wa hatari na wa kupanua mipaka wa utawala wa Kizayuni. Lazima tukabiliane nao kwa kila njia na mbinu. Adui huyu haheshimu makubaliano yoyote.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem, amesema kuwa Lebanon inakabiliwa na uvamizi wa hatari na wa kupanua mipaka wa utawala wa Kizayuni, na akasisitiza kuwa uvamizi huo lazima ukabiliwe kwa kutumia mbinu na nyenzo zote zinazowezekana.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa hafla kubwa ya “Najee’ wa Midad”, iliyofanyika leo katika makaburi ya Kiongozi wa Harakati ya Upinzani, Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, kusini mwa Beirut, kwa lengo la kuwakumbuka wanazuoni mashahidi wa njia ya Quds na mapambano ya Kiislamu.

Mashahidi 15 ambao ni Maulamaa, 41 wakiwa ni wanafunzi Dini, na watoto 39 wa Maulamaa

Sheikh Naim Qassem alisema: “Tumeikusudia hafla hii kwa ajili ya kuwakumbuka Wanazuoni Mashahidi. Tunataka kufahamu kwa undani mkondo huu mkubwa uliobadili maisha yetu.”

Alifafanua kuwa jina la tamasha hilo ni “Najee’ wa Midad”, / جميع ومِدادٌ ambapo:

  • 1_Najee humaanisha damu
  • 2_Midad humaanisha wino wa elimu

Akaongeza: “Leo damu ya wanazuoni mashahidi imezaa matunda, na sasa ni wakati wa kuvuna. Walikuwa ndio waliopanda mbegu ardhini kwa jitihada zao, na wakaleta mvua ya baraka kutoka mbinguni.”

Kwa mujibu wa takwimu alizozitaja:

  • 1_Maulamaa mashahidi wenye majoho ni 15
  • 2_Wanafunzi wa vyuo vya dini waliouawa ni 41
  • 3_Watoto wa wanazuoni waliouawa ni 39.

Sayyid Abbas Mousawi na Sheikh Ragheb Harb walikuwa vinara wa njia ya shahada

Sheikh Naim Qassem alisisitiza umuhimu wa kuwakumbuka:

  • 1_Sayyid Abbas Mousawi
  • 2_Sheikh Ragheb Harb

Akasema:
“Hawa wawili walikuwa ndio vinara wa mwanzo katika njia ya shahada na jihadi.”

Alibainisha kuwa: “Jihadi ni msingi wa mfumo wa Uislamu. Tuna jihadi mbili:

  • 1_Jihadi ya kujisafisha nafsi
  • 2_Na jihadi ya kijeshi.”

Hezbollah ni mradi wa heshima, uhuru na maadili

Sheikh Naim Qassem alieleza kuwa watu wengi walishangazwa na mafanikio ya Hizbullah kubadili mwelekeo wa mapambano ya Lebanon, akisema: “Kazi yetu ndani ya Hizbullah inasimamia ukamilifu wa dini. Tumeshikamana na misingi ya Uislamu na tunaamini jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ndiyo mafundisho ambayo wanazuoni wetu waliidhihirisha.”

Aliongeza kuwa: “Walitaka kuuangamiza mradi wa Hizbullah kwa sababu unatetea taifa, uhuru, heshima na maadili. Wao hawataki tuishi maisha yenye heshima.”

Muungano wa Hezbollah na Wakristo mwaka 2006

Sheikh Naim Qassem alikumbusha kuwa: “Mwaka 2006 Hizbullah iliunganisha nguvu na harakati kubwa ya Kikristo - Harakati ya Uhuru wa Kitaifa - na hivyo kutoa mfano wa umoja wa kitaifa unaovuka mipaka ya dini.”

Lebanon inakabiliwa na uvamizi hatari wa Kizayuni

Akirejea mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel kusini mwa Lebanon, alisema:

Lebanon inakabiliwa na uvamizi wa hatari na wa kupanua mipaka wa utawala wa Kizayuni. Lazima tukabiliane nao kwa kila njia na mbinu. Adui huyu haheshimu makubaliano yoyote.”

Akaongeza kwa msisitizo: “Hakuna mtu yeyote duniani anayeweza kutunyima uwezo wetu wa kujilinda.”

Marekani na Israel hazina haki ya kuingilia silaha na ulinzi wa Lebanon

Sheikh Naim Qassem alisema: “Marekani na Israel hazina haki ya kuingilia maamuzi ya Lebanon kuhusu silaha na mkakati wa ulinzi. Makubaliano ya kusitisha mapigano yanahusu tu eneo la kusini mwa Mto Litani.”

Alisisitiza: “Wanataka kufuta kabisa uwepo wetu. Lakini tutajilinda sisi, familia zetu na nchi yetu, na tuko tayari kujitolea kwa ajili ya Msikiti wa Al-Aqsa. Hatutasalimu amri.”

Ushirikiano wa Hizbullah na serikali ya Lebanon utaendelea

Mwisho, Katibu Mkuu wa Hizbullah alisema: “Tutaendelea kushirikiana na serikali ya Lebanon katika njia ya diplomasia iliyoichagua. Hatutawajali watumishi wa Marekani na Israel.”

Akaongeza: “Tunaitarajia serikali yetu ionyeshe ujasiri wake mbele ya uvamizi wa Kizayuni, katika ukombozi wa mateka na katika ujenzi upya wa nchi.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha